Himdi zote anastahiki Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, na rema na amani zimshukie mtume mbora zaidi. Baada ya hayo…
Ndugu msomaji mpenzi,
Kurani Tukufu ni neno la Mwenyezi Mungu alilomshushia Mtume wake Muhammad ﷺ ili kuwatoa watu kutoka gizani na kuwaleta kwenye nuru. Ni muujiza katika matamshi na maana zake, na kuisoma ni ibada. Ni kitabu cha mwisho na kilichokamilika zaidi miongoni mwa vitabu vya mbinguni, na Mwenyezi Mungu amemwamuru Mtume wake ﷺ kukifikisha kwa walimwengu wote.
Mwenyezi Mungu amejitwalia jukumu la kukilinda, na ameweka ndani yake nguvu ya ushawishi inayovuta masikio, akili, nyoyo na roho. Pamoja na hayo, wasio Waislamu wengi hawapati fursa ya kusoma Kurani nzima, na hata wakipenda, wanaweza kuchanganyikiwa waanzie wapi.
Kwa sababu hiyo, kupitia tovuti hii tumejitahidi kuchagua aya teule zinazoelezea mada kuu katika Uislamu, kama vile:
Lengo letu katika uchaguzi huu ni kurahisisha uelewa wa ujumbe wa Uislamu, na si kuchukua nafasi ya kusoma Kurani nzima, bali tunatumai hii itakuwa hamasa ya kuisoma yote.
Tunamwomba Mwenyezi Mungu Aliyetukuka aijaalie kazi hii kuwa kwa ajili yake Yeye pekee, na iwe sababu ya uwongofu wako, kuingia kwako Peponi, na kukulinda na adhabu ya Moto.
❝Basi mkumbushe kwa Kurani yule anayeogopa maonyo Yangu.❞ [Qaf: 45] ❝Ametukuka Yule aliyeteremsha Furqani (Kurani) kwa mja wake ili awe mwonyaji kwa walimwengu wote.❞ [Al-Furqan: 1]
Na rehma na amani zimshukie Mtume wetu Muhammad, familia yake, na masahaba zakwe wote.